Ijumaa, 24 Juni 2016

HYDROPONIC FODDER

Muendelezo........
HYDROPONIC TEKNOLOJIA UNAYOWEZA KUIFANYA HATA NYUMBANI.
Baada ya kuwa umeandaa vifaa vyako tayari,hatua inayofuata ni uoteshaji.
JINSI YA KUOTESHA.
   Mbegu unazoweza kuotesha ni kama vile:mahindi,shayiri,mtama,ngano no.MBEGU HIZI HUOTESHWA KULINGANA NA AINA YA MIFUGO.
  Ili kupata matokeo mazuri katika kuwalisha kuku,inashauriwa uoteshe NGANO au SHAYIRI.
   Ikumbukwe kuwa kilogramu 1 ya ngano inaweza kulisha kuku 100 kwa siku moja.Hivyo otesha kulingana na idadi ya kuku ulionao.
    HATUA ZA UOTESHAJI.
1:Anza kupembua mbegu zako,hakikisha unaondoa zote zisizofaa.
2:Chukua mbegu nzuri kisha ziweke ndani ya maji safi.
3:Ondoa mbegu zitakazopanda juu.
4:Ondoa mbegu zilizobaki chini ya maji.
5:chukua JIK kifuniko kimoja changanya kwenye maji lita tatu, mchanganyiko huu ni kwa kila kilogramu moja ya mbegu.
6:Dumbukiza mbegu kwenye mchanganyiko huo,kisha ziache kwa nusu SAA.
7:Baada ya mda huo zioshe kwa maji hayo.
8.Toa mbegu na uzioshe mara mbili kwa maji safi.
9:Chukua mbegu na uziweke ndani ya ndoo yenye matundu madogomadogo chini. Kisha funika juu kwa kitambaa kisafi.
10:Nyeshelea kwa maji yenye mchanganyiko wa HYDROPONIC NUTRIENTS mara tatu kwa siku.Na kinga maji yatakayotoka kwa chini, unaweza kuyatumia kunyeshea kwa wakati mwingine.
11.Ziache kwenye ndoo siku mbili.Kisha zitoe na uzisambaze kwenye trei.
12:Funika kwa siku moja juu ya trei kutumia kitambaa kisafi.nyeshelea mara tatu kwa siku.
13:Ondoa kitambaa juu ya trei na endelea kunyeshea hadi siku ya tano.
Itakuwa tayari kuvunwa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Maoni 3 :

  1. Naomba kuuliza Masaaki kidogo. JIK mnayozungumzia ni ile ya kufulia nguo? Hizo Nutrients nazipata wapi? Kwanini tunatumia JIK? Kwa sasa notes ha kwenye mfuko wa Salfet tu ila kunachangamoto. Mudyabbas@gmail.com

    JibuFuta
  2. Naomba kuuliza Masaaki kidogo. JIK mnayozungumzia ni ile ya kufulia nguo? Hizo Nutrients nazipata wapi? Kwanini tunatumia JIK? Kwa sasa notes ha kwenye mfuko wa Salfet tu ila kunachangamoto. Mudyabbas@gmail.com

    JibuFuta
  3. Jik tunatumia ya nyumbani,tunatumia Jiki kuondoa sumu za madawa zilizopuliziwa mbegu,
    PIGA:0712815848 KWA MAHITAJI YA NUTRIENTS

    JibuFuta