Ufugaji!
Hii ni dhana pana zaidi inayogusa maisha ya watu wengi zaidi katika maisha yetu kwa sasa!
Wengi wanavutiwa sana kufuga iwe ni kuku,bata, Ng'ombe nk.Zamani ufugaji ulikuwa kama shughuli kuu katika jamii.Lakini baada ya maendeleo na mabadiliko katika nyanja mbalimbali za kiuchumi,sekta hii ilianza kupuuzwa katika jamii nyingi za Africa.
Lakini sasa imeanza kurudi kupendwa na wanajamii,katika kurudi huko imekutana na 'Ukisasa'yani imefanywa katika njia yenye maboresho zaidi.
Leo tofauti na miaka mingi iliyopita kuna uwezekano wa kufuga katika eneo dogo na kupata faida,kuna madawa ya kisasa za mifugo,mbegu zilizoboreshwa zaidi na zenye faida kubwa.Hii yote ni katika kuona Kuwa mfugaji ananufaika maradufu.
Kiukweli ni jambo jema kuwa na mabadiliko kama hayo.Lakini mabadiliko haya yanaonekana kuwa na faida zinazomnufaisha zaidi muuzaji kuliko yule anayekwenda kutumia.
Miaka mingi iliyopita ilikuwa ni ngumu kukutana na kuku anayekuwa kwa wiki 3-4na afae kuuza tayari kwa kuliwa.Leo ndio wamejaa mtaani zaidi ya kuku wa asili tulio wazoea.Lakini pia hata kukuwa asili tuliowazoea leo wanafugwa kisasa zaidi jambo ambalo linasababisha madhara kwa walaji japokuwa ni lenye faida kwa wauzaji.
Kwa kawaida kuku wa kienyeji hujitafutia chakula kwa 75% na zilizobaki 25% hupata toka kwa mfugaji wake.Leo inasikitisha kwa kuwa mfugaji humlisha kuku wake kwa 98% na zilizobaki 2% ndizo hujitafutia mwenyewe.Hii imesababisha kupoteza uasilia wa kuku hawa na kuwa kama kuku wa kisasa.Leo ni rahisi zaidi kumpata kuku wa kienyeji mwenye nyama nyeupe(hii husababishwa na aina ya chakula anachopatiwa)tofauti na tulivyozoea kuku hawa kuwa na nyama yenye 'unjano' .
"Kuku aliyefugwa miaka 40 iliyopita ni tofauti sana na kuku wa leo, kuku wa sasa ana mafuta mara 266 zaidi ya yule aliyefugwa miaka 40 iliyopita.Mafuta hayo sio ya asili"(Ripoti ya shirika la afya duniani).
Ingawaje kufuga kisasa ni muhimu ila kuendane pamoja na kujali afya za walaji.
UNAWEZA KUWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI!
Ili kuwa wa kwanza kupata kila habari inayotumwa bonyeza neno "Follow" linalooneka juu kulia mwa ukurasa huu.
Kwa ushauri zaidi juu ya ufugaji bora
Wasiliana na:
Patrick Roman
+255712815848
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni