Jumamosi, 19 Novemba 2016

NI KILIMO AU UFUGAJI TANZANIA?

Na *Patrick Roman*

Napenda kukuandikia.
Ni katika pitapita nakutana na mfugaji huko Ethiopia jina lake ni Kaamila,n mama wa watoto kadhaa,mfugaji mdogo.

Nchini Ethiopia hichi ni kipindi cha kiangazi chenye ukame mkubwa unaomlazimu mfugaji huyu kutafuta malisho kwaajili ya ng'ombe wake.
Anasema kuwa katika kipindi kama hichi yeye huamua kutembea umbali wa siku 3 hadi katika maeneo ya milima ili kupata maeneo ya malisho kulisha ng'ombe wake.Watoto wake hulazimika kutoenda shule kwa muda wote wa ukame ili waandamane na mama yao, kwa kuwa hakuna wa kubaki nyumbani.

"Ni kipindi kigumu sana kwangu,familia,na mifugo yangu,tunalala katika vichaka,tunatembea umbali mrefu ili kuhakikisha tunapata malisho" anasema Kaamila

Kaamila ni miongoni mwa wafugaji na wakulima wanaopitia halingumu Afrika. Bado hawajanufaika na Kazi zao, mabadiliko ya teknolojia hayajawagusa.
Hali kama za Kaamila ndizo zinazopelekea kukata tamaa kwa wengi wetu katika maswala ya Kilimo na Ufugaji.

Wewe unamaoni gani katika kurudisha hamasa na kutatua changamoto hzi????????
Kumbuka:������������
Green Tanzania Youth Movement,COMING SOON!��������

Jumapili, 21 Agosti 2016

UJUE UGoNJWA WA UKOSEFU WA BIOTIC(VITAMINI)

Habari za muda huu msomaji mpendwa wa makala zangu?
Katika harakati za kuendelea kukuza sekta ya ufugaji nchini Tanzania,leo nimeona nikuletee moja ya ugonjwa unaosumbua.
UKOSEFU WA VITAMINI!
Ugonjwa huu upata kuwa wa mwezi 1 na mara nyingine miezi 3.Huathiri baadhi ya kuku katika banda na mara nyingine hupelekea vifo.
Ikiwa utawahiwa unaweza kutibika na kuku kurudia katika hali yake.

DALILI!
-Kuku kulegea na kukosa nguvu katika miguu na shingo.
-Shingo kupinda.
-Kuku kujizungusha na kujupiga piga.
-kushindwa kutoa kinyesi kwa muda mrefu na kinapotoka huwa kikubwa.
-kuku hushindwa kula

SULUHISHO
Ili kuwakinga kuku wako na ugonjwa huu kumbuka kuwapatia dawa iliyokatika mfumo wa 'multivitamin' wanapokuwa wamefikisha siku ya 14 toka kutotolewa.
Au ikiwa kuku wàtakuwa wameathirika wapatie 'multivitamin' zenye mchanganyiko wa BIOTIC mara tu unapogundua tatizo.
Pia wapatie DCP ili kuimarisha mifupa na misuli yao.
Kumbuka kuwalisha kuku wagonjwa wakati wanapokuwa wanaumwa.

DAWA
*Broiler boost multivitamin nk.



Tuwekee maoni yako hapa chini.
Ushauri zaidi:-
Piga:+255712815848
Imeandaliwa na:Patrick Roman

UFUGAJI WA KISASA USIVYOJALI AFYA YA MLAJI!!

Ufugaji!
Hii ni dhana pana zaidi inayogusa maisha ya watu wengi zaidi katika maisha yetu kwa sasa!
Wengi wanavutiwa sana kufuga iwe ni kuku,bata, Ng'ombe nk.Zamani ufugaji ulikuwa kama shughuli kuu katika jamii.Lakini baada ya maendeleo na mabadiliko katika nyanja mbalimbali za kiuchumi,sekta hii ilianza kupuuzwa katika jamii nyingi za Africa.
Lakini sasa imeanza kurudi kupendwa na wanajamii,katika kurudi huko imekutana na 'Ukisasa'yani imefanywa katika njia yenye maboresho zaidi.
Leo tofauti na miaka  mingi iliyopita kuna uwezekano wa kufuga katika eneo dogo na kupata faida,kuna madawa ya kisasa za mifugo,mbegu zilizoboreshwa zaidi na zenye faida kubwa.Hii yote ni katika kuona Kuwa mfugaji ananufaika maradufu.
Kiukweli ni jambo jema kuwa na mabadiliko kama hayo.Lakini mabadiliko haya yanaonekana kuwa na faida zinazomnufaisha zaidi muuzaji kuliko yule anayekwenda kutumia.
Miaka mingi iliyopita ilikuwa ni ngumu kukutana na kuku anayekuwa kwa wiki 3-4na afae kuuza tayari kwa kuliwa.Leo ndio wamejaa mtaani zaidi ya kuku wa asili tulio wazoea.Lakini pia hata kukuwa asili tuliowazoea leo wanafugwa kisasa zaidi jambo ambalo linasababisha madhara kwa walaji japokuwa ni lenye faida kwa wauzaji.
Kwa kawaida kuku wa kienyeji hujitafutia chakula kwa 75% na zilizobaki 25% hupata toka kwa mfugaji wake.Leo inasikitisha kwa kuwa mfugaji humlisha kuku wake kwa 98% na zilizobaki 2% ndizo hujitafutia mwenyewe.Hii imesababisha kupoteza uasilia wa kuku hawa na kuwa kama kuku wa kisasa.Leo ni rahisi zaidi kumpata kuku wa kienyeji mwenye nyama nyeupe(hii husababishwa na aina ya chakula anachopatiwa)tofauti na tulivyozoea kuku hawa kuwa na nyama yenye 'unjano' .
"Kuku aliyefugwa miaka 40 iliyopita ni tofauti sana na kuku wa leo, kuku wa sasa ana mafuta mara 266 zaidi ya yule aliyefugwa miaka 40 iliyopita.Mafuta hayo sio ya asili"(Ripoti ya shirika la afya duniani).
Ingawaje kufuga kisasa ni muhimu ila kuendane pamoja na kujali afya za walaji.
UNAWEZA KUWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI!
Ili kuwa wa kwanza kupata kila habari inayotumwa bonyeza neno "Follow" linalooneka juu kulia mwa ukurasa huu.
Kwa ushauri zaidi juu ya ufugaji bora
Wasiliana na:
Patrick Roman
+255712815848

Jumanne, 16 Agosti 2016

FANYIA KAZI HAYA KABLA HUJAANZA KUZALISHA CHOCHOTE!

 1.UKOSEFU WA MAARIFA SAHIHI
-Ni vizuri ikafahamika kuwa kilimo ni utaalamu kabisa (Sayansi) kama ilivyo udaktari au uhandisi au fani yoyote ile inayohitaji maarifa.Ndio maana mimea usipojua mahitaji yake kwa wakati sahihi, baadhi itakufa, au itakuletea mavuno hafifu, n,k
Hivyo kabla ya kwenda shambani na kuwekeza muda wako na pesa zako, ni muhimu sana KWANZA ukajifunza kupata maarifa sahihi ya kitu gani unataka kuzalisha, mbegu gani utatumia, madawa (WADUDU &UKUNGU), mbolea, wadudu gani waharibfu utakabiliana nao vipi, utahifadhi vipi mazao yako baada ya kuvuna na mambo mengine mengi.
BILA KUFANYA HIVYO UTAPATA HASARA TU, kwa sababu sasa hivi kilimo ni soko huria, hivyo utakutana na pembejeo feki nyingi sana za kilimo humo madukani, wauzaji na wasambazaji BAADHI SI WAAMINIFU (ANZIA MBEGU, MADAWA, MBOLEA).
Utapanda mbegu feki hazitaota, utatumia madawa feki yata kuunguzia mimea yako, na wakati mwingine utauziwa madawa hata iaina 5 yanayofanya kazi mmoja ya kuua wadudu (hivyo kupoteza fedha zako). Ukisosa maarifa sahihi utakuwa mtu wa kutanga tanga tu, kwa mfano wakati wa kuweka mbolea ya kukuzia wewe unaweka mbolea ya kupandia, wakati yan kuweka dawa za kukinga mimea yako na ukungu wewe unaweka dawa za kuua wadudu, aina fulani ya dawa hazifai kuua magugu ukiwa umeshapanda mimea wewe utatumia tu kiua gugu chochote herbicides bila kujua ipi inafaa wakati gani, hivyo utapoteza pesa zako nyingi kwa kutanga tanga na kutokujua ufanye nini kwa wakati sahihi
-Jambo lingine sambamba na maarifa, ni kuwa UNAPASWA KUANZIA SOKONI KWANZA KABLA YA KUZALISHA ZAO LOLOTE LILE, LENGO NI UJUE
i). NI ZAO GANI LINAKUWA ADIMU/
LINAPENDWA SOKONI (WALAJI) WAKATI GANI LINAKUWEPO SOKONI KWA WINGI AU LINAKUWA NA MAHITAJI MAKUBWA-
Lengo la kutambua hili ni Ili sasa ukajipange kuzalisha kuendana na mahitaji ya soko, ili huo wakati uatao vuna na kupeleka sokoni ukutane na bei nzuri kwa maana ya demand and supply-kama mzigo upo kidogo sokoni na mahitaji ni makubwa automatically bei itakuwa juu na hivyo kuwa faida kwako wewe mzalishaji.
Mfano kwa uzoefu wangu- nafahamu mazao mengi sana huwa adimu sokoni kuanzia miezi ya disemba hadi April maana mvua huwa nyingi nyakati hizo hivyo wengi huogopa kuzalisha wakati huo kuhofia mafuriko, wadudu na magonjwa ya ukungu ni mengi sana, na hapo ndio bei za vyakula huwa juu, hivyo ukiweza kutime nyakati hizo lazima utapata faida
ii). NI MUHIMU PIA KUTAFITI, ni aina ipi ya hilo zao linapendwa sana na walaji, mfano je walaji wanapenda nyanya size nene sana, au saizi ya kati au ndogondogo, au mfano katika matikiti je wanapenda ya rangi zenye michirizi maarufu kama zebra, au ya kawada, je katika Karoti wanapenda karoti fupi nene, au nyembamba ndefu, au mfano katika kabichi walaji/soko wanapenda za iana gani zenye ngozi ngumu na umbo kubwa (kilo 4-7 etc) au saizi ndogo? etc.
2. UKOSEFU WA MAANDALIZI SAHIHI (MTAJI)
Wakulima wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa hawakujipanga, kuanisha mahitaji mahususi yanayotakiwa katika kilimo husika, hawakujipanga vizuri kukabiliana na changamoto mbalimbali, Mfano- (Mkulima hakupiga mahesabu sahihi ya mahitaji ya shamba lake tangu kuandaa shamba, kupanda, mbegu madawa, mbolea, palizi, mavuno, hadi kufikisha sokoni) anapoanza kilimo akikutana na changamoto mfano za mbolea za kupandia, kukuzia, au za maua na matunda (booster), pesa inakata naye anakata tamaa anaamua kuzalisha tu ili mradi au kutelekeza mashamba, hivyo ni muhimu sana , kujipanga kabla ya kuanza shughuli yoyote, ambayo utajitoa muda wako na pesa yako.

MJUE BATA BUKINI KWA UFUGAJI WENYE MAFANIKIO

BATA BUKINI
UFUGAJI WENYE TIJA
Tofauti na ndege wengine au bata wengine wa kawaida, mfugaji wa bata bukini anaweza kupata kipato kikubwa kwa haraka na kwa gharama ndogo.
Bata Bukini ni ndege ambao asili yao ni India na Japan. Hii ni jamii ya ndege wafugwao lakini tofauti kubwa ya bata wa kawaida wao wana asili ya usafi, hivyo hawapendi uchafu na kamwe hawali mizoga.
Kuna aina mbili ya bata bukini ambao ni weupe na wenye mchanganyiko wa rangi. Hali kadhalika hutofautiana katika utagaji wa mayai.
CHAKULA
Ndege hawa wanakula chakula kama wanacholishwa kuku, wanapendelea kula majani jamii ya mikunde kwa 50% na hawahitaji chakula kingi. Vifaranga ni lazima wapatiwe lishe kamili hasa protini kwa wingi ili waweze kujenga mwili, kukua vizuri na kuwa na afya nzuri.
Kwa maana hiyo, vifaranga wanahitajika kupata walau 20% ya protini kwa wiki mbili za awali na baada ya hapo waweza kupunguza hadi 15% kulingana na kukua kwao hadi wanapokuwa wanaelekea kukomaa.
Kama ambavyo mfugaji anaweza kutengeneza chakula kwa ajili ya mifugo wengine, pia anaweza kutengeneza cha bata bukini kama ifuatavyo:
Mahitaji
🐥 Mahindi kilo 10 ( hakikisha hayana dawa)
🐥 Chokaa kilo 5 (ya kulishia mifugo)
🐥 Dagaa kilo 10 (wanaotumika kulishia kuku)
🐥 Mashudu kilo 20
Utengenezaji na Uhifadhi
Baada ya kupima vyakula hivi kwa usahihi chukua pipa, changanya vizuri kisha walishe bata kulingana na wingi wao na uhakikishe wanapata chakula cha kutosha. Vipimo hivi hutegemea wingi wa bata unaowafuga lakini hakikisha uwiano huo unazingatiwa. Baada ya kutengeneza chakula unaweza kuhifadhi katika mifuko na kuweka katika eneo lisilokuwa na unyevu.
Kuatamia
Jinsi ilivyotofauti katika idadi ya utagaji wa mayai hivyo ndivyo uwezo wa kuatamia pia ulivyo. Bata Bukini weupe huatamia mayai 6 na wale wa rangi huatamia mayai 12
Ndege hawa huatamia kwa siku 29, huangua vifaranga kwa siku 3 na mara nyingi hutotoa mayai yote, si rahisi mayai kubaki bila kutotolewa au kuharibika.
Namna ya kutunza vifaranga
Mara tu vifaranga wanapoanguliwa, wachukue na kuwatenga na mama yao kisha waweke katika banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya umeme kama una uwezo ili kuwatengenezea joto.
Pia, waweza kuzungushia banda lao kitu kizito kama blanketi ili kuwakinga na baridi au upepo.
Banda
Bata Bukini wanahitaji nafasi ya kutosha hivyo andaa banda kulingana na wingi wa bata unaotarajia kufuga.
Hakikisha banda limesakafiwa au banda la udongo lisilotuamisha maji au unaweza kuweka mbao au mabanzi kisha unaweka maranda ili kuwakinga na baridi.
Maji
Ni lazima bata wapatiwe maji ya kunywa kila siku na hakikisha banda halikosi maji wakati wote. Safisha chombo cha maji na kubadilisha maji kila siku.
Ndege hawa wanahitaji maji ya kunywa ya kutosha kama ilivyo kwa kuku. Hakikisha maji yako kwenye chombo ambacho hayatamwagika , kwani kumwagika kunaweza kusababisha kuibuka kwa magonjwa.
Bata Bukini hawapendi uchafu. Hivyo maji yawe mahali ambapo hayatachafuka.
Magonjwa
Ni mara chache sana bata bukini kushambuliwa na magonjwa kama watawekwa katika hali ya usafi. Magonjwa yanayoweza kuwasumbua ni mafua na wakati mwingine kuharisha.
Tiba za asili
Unaweza kutibu bata bukini kwa njia za asili. Tumia mwarobaini, vitunguu (maji na saumu).
🌑 Mwarobaini: unaweza kutumia dawa hii kutibu mafua kwa bata bukini wakubwa au vifaranga.
Maandalizi
Chukua kiasi kidogo cha mwarobaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji ya mwarobaini, kisha changanya na maji uliyo andaa kuwanywesha vifaranga.
🌑 Kitunguu Saumu na Kitunguu Maji:
Dawa hii hutumika kukinga na kutibu bata bukini wanaoharisha.
Maandalizi
Unachukua kitunguu saumu au maji na kuondoa maganda ya nje kisha safisha na kukata vipande vidogovidogo na kuwawekea kama chakula.
Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapopona.
🌑 Majani: Bata Bukini chakula chao kikubwa ni majani. Majani yana vitamini A, hivyo hakikisha unawapatia ya kutosha. Wapatie majani jamii ya mikunde.
KUTAGA
Bata Bukini huanza kutaga baada ya miezi saba na hutaga mara tatu kwa mwaka. Isipokuwa, utagaji wa bata bukini weupe na wa rangi hutofautiana katika idadi ya mayai
Bata Bukini weupe hutaga mayai sita tu lakini wale wa mchanganyiko wa rangi hutaga mayai kumi na mbili (mara mbili ya bata weupe).

Ijumaa, 5 Agosti 2016

KILIMO CHA MATANGO FURSA NYINGINE YA UTAJIRI

Matango (cucumber) ni zao muhimu katika mazao ya mboga na matunda nchini Tanzania na hata nje ya Tanzania.
Ni vizuri kuwekea matango fito kwani matunda yake yakilala ardhini huoza.
Hili ni zao la biashara, pia chakula. Zao hili hustawi na kulimwa kwa wingi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Pwani.

Matumizi: Matango hutumika kama tunda, ijapokuwa ni aina ya mboga na huongeza vitamin A, C na maji mwilini. Pia, tango linaweza kutumiwa kama saladi wakati wa mlo.

Hali ya hewa:

Matango hustawi kwenye hali ya joto, hali kadhali kwenye sehemu yenye joto kidogo pia hustawi. Matango yanahitaji joto wastani wa nyuzi joto 20°C – 25°C. Zao hili pia huhitaji maji kwa wingi, ingawa unyevu ukizidi husababisha magonjwa kwenye majani na maua.



Udongo:
 Kwa ustawi mzuri wa matango, udongo unatakiwa kuwa na rutuba ya kutosha, na chachu ya kuanzia 5.5 hadi 6.7, mwinuko unaotakiwa ni kuanzia mita 1000-1200 kutoka usawa wa bahari.

Tofauti na ilivyo mazao mengine, matango hayahitaji mwanga mkali sana kwa kuwa husababisha maua dume kuzaliwa, hivyo kuathiri uzalishaji wa idadi ya matunda ya matango. Mwanga kidogo husababisha maua jike kuchanua kwa wingi kuongeza kiwango cha mazao. Mwanga unapokuwa mwingi, inabidi kutumia neti au aina nyingine ya vizuizi ili kupunguza mwanga, ambapo pia itasaidia kulinda mmea dhidi ya upepo mkali ambao unaweza kuharibu maua na matunda, au mmea kwa ujumla.

Kupanda:

Mara nyingi matango hupandwa moja kwa moja shambani. Wakulima wengine hupanda kwenye vitalu au makopo na baadae kuhamishia miche inapofikia sentimita 8-12. Endapo mbegu zimepandwa shambani moja kwa moja, inatakiwa ipunguzwe na kubakia mche mmoja tu kwenye kila shimo.

Nafasi:

Nafasi kati ya mche na mche ni sentimita 60-70, na nafasi kati mstari na mstari ni sentimita 70-90. Mimea inatakiwa iwekewe miti ili iweze kuzaa matunda mengi na kuepuka kukaa chini ambapo matunda yanaweza kuoza au kuharibiwa na wadudu.

Mbolea:

Mbolea ni muhimu sana, kabla ya kupanda au kuhamisha miche. Mbolea inayoweza kutumika ni samadi au ya viwandani isiyokuwa na madhara kwa mazingira na afya ya binadamu. Baada ya kupanda, tumia mbolea ya maji maji kila baada ya siku 14-21, mpaka mmea uweke matunda.

Palizi:

Palizi ni muhimu , ili kuepuka magonjwa na kunyang’anyana chakula kati ya zao na magugu.

Wadudu waharibifu: Wadudu waharibifu wa matango ni pamoja na Vidukari, inzi weupe, na minyoo ya mizizi.

Magonjwa:

Magonjwa yaliyozoeleka kushambulia matango ni pamoja na Ukungu, fusari, na magonjwa ya virusi.

Kuvuna:

Matango yanaweza kuwa tayari kuvunwa kuanzia siku 50-60 na matunda yanatakiwa yawe na urefu wa sentimita 15 mpaka 20. Makadirio ya mavuno ni tani 6 kwa ekari moja.

Kadirio la gharama:

Hebu tuangalie kwa Makadirio tuu ya gharama za kuzalisha walau nusu ekari ya Tango.

1. Mbegu hybrid F1 = Tsh. 180,000/=
2. Kulima 30,000/=
3. Dawa 40,000/=
4. Palizi 30,000/=
5. Mbolea 120,000/=
JUMLA = 400,000/=

Lakini hizi zinatofautiana na maeneo.

Toa maoni

Alhamisi, 14 Julai 2016

KUROILER MKOMBOZI WA MFUGAJI

Kuku bora kwa sasa ni KUROILER.Ana uzito wakutosha,anaimili magonjwa,anafugwa hata kienyeji,hutaga akiwa na miezi 4,akiwa na miezi 4 jogoo hufikia uzito wa 5kg na mtetea 3.5kg,anataga mayai mengi.
Jamii hii asili yake ni India,ndiyo jamii ya kuku iliyofugwa India ili kupambana na umaskini,kutokana nafaida hizo hapo juu ndio sababu wakaonekana kuwa suluhisho la umaskini.
Anza nawe kufuga aina hii kwa matokeo makubwa ya mapinduzi katika ufugaji.